# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Kwa mwanamuziki mkuu "Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu" # kwenye vyombo vya nyuzi "watu wanapaswa kucheza vyombo vya nyuzi na wimbo huu" # kusababisha uso wake ung'ae kwetu Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwatendea fadhila kana kwamba uso wa Yahwe uling'aa mwanga juu yao. "kututendea fadhili" # njia zako zijulikane duniani Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu wajue njia zako duniani" # wokovu wako miongoni mwa mataifa yote Mwandishi anatamani kila mtu ajue kuwa Mungu ana uwezo wa kuwaokoa. Hii inaweza kuwekwa wazi. "na watu wa mataifa yote wajue kuwa una uwezo wa kuwaokoa"