sw_tn/psa/032/007.md

28 lines
1.1 KiB
Markdown

# Wewe ni maficho yangu
Yahwe anazungumziwa kana kwamba ni sehemu salama dhidi ya mashambulizi ya adui wa mwandishi. "Wewe ni kama sehemu ambayo naweza kujificha dhidi ya adui zangu"
# Utanizunguka na wimbo wa ushindi
Sitiari hii inamaanisha kuwa ulinzi wa Yahwe kwa mwandishi ndio sababu ya nyimbo za ushindi alizoimba. "Kwa sababu yako nitaimba nyimbo za ushindi"
# Sela
Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kihebrabia, na zingine haziliweki.
# Nitakuelekeza na kukufundisha katika njia
Maneno "kuelekeza" na "kufundisha" zinamaana sawa na zinasisitiza maelekezo makini. "Nitakufundisha kila kitu kuhusu njia"
# Nitakuelekeza
Hapa anayesema hivi ni Yahwe akimwambia Daudi.
# katika njia unayopaswa kwenda
Kuishi katika njia sahihi inazungumziwa kana kwamba ni njia ambayo mwandishi anapaswa kutembea. "jinsi ya kuishi maisha yako"
# na jicho langu juu yako
Hapa "jicho langu" linamaanisha Yahwe kuzangatia kwa umakini. "na kuweka umakini wangu kwako" au "kukuangalia"