# Wewe ni maficho yangu Yahwe anazungumziwa kana kwamba ni sehemu salama dhidi ya mashambulizi ya adui wa mwandishi. "Wewe ni kama sehemu ambayo naweza kujificha dhidi ya adui zangu" # Utanizunguka na wimbo wa ushindi Sitiari hii inamaanisha kuwa ulinzi wa Yahwe kwa mwandishi ndio sababu ya nyimbo za ushindi alizoimba. "Kwa sababu yako nitaimba nyimbo za ushindi" # Sela Hili linaweza kuwa neno la kimuziki linalowaongoza watu jinsi ya kuimba au kujecheza vyombo hapa. Tafsiri zingine huandika neno hili la Kihebrabia, na zingine haziliweki. # Nitakuelekeza na kukufundisha katika njia Maneno "kuelekeza" na "kufundisha" zinamaana sawa na zinasisitiza maelekezo makini. "Nitakufundisha kila kitu kuhusu njia" # Nitakuelekeza Hapa anayesema hivi ni Yahwe akimwambia Daudi. # katika njia unayopaswa kwenda Kuishi katika njia sahihi inazungumziwa kana kwamba ni njia ambayo mwandishi anapaswa kutembea. "jinsi ya kuishi maisha yako" # na jicho langu juu yako Hapa "jicho langu" linamaanisha Yahwe kuzangatia kwa umakini. "na kuweka umakini wangu kwako" au "kukuangalia"