sw_tn/psa/032/001.md

28 lines
932 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Zaburi ya Daudi
Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.
# Maschili
Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.
# ambaye makosa yake yamesamehewa, ambaye dhambi zake zimefunikwa
Misemo hii ina maana ya kufanana. Inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambaye Mungu husamehe makosa yake na kufunika dhambi zake"
# dhambi zake zimefunikwa
Hapa dhambi iliyosamehewa inazungumziwa kana kwamba imefunikwa ili isionekane. "ambaye dhambi yake haijaliwi" au "ambaye dhambi yake inasahauliwa makusudi"
# ambaye Yahwe hamhesabii hatia
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "ambaye Yahwe anaona hana hatia" au "ambaye hana hatia kulingana na Yahwe"
# ambaye rohoni mwake hakuna hila
Hapa "roho" inamaanisha mtu. "ambaye hakuna hila" au "ambaye ni mkweli kabisa"