sw_tn/psa/025/004.md

16 lines
555 B
Markdown

# Unijulishe njia zako, Yahwe; nifundishe njia zako
Kauli hizi mbili zina maana moja. Mungu kumfundisha mtu jinsi anavyotakiwa kutenda inazungumziwa kana kwamba alikuwa akimwonyesha mtu njia sahihi ambayo mtu anapaswa kusafiria.
# Nakutumaini
"Nakutegemea" au "Nakusubiri kwa uvumilivu"
# Niongoze kwenye kweli yako na unifundishe
Niongoze na unifundishe zina maana sawa, kutoa maagizo. "Nielekeze kusimamia maisha yangu kwa kutii ukweli wako"
# Mungu wa wokovu wangu
Nomino dhahania ya "wokovu" inaweza kuelezwa kama "'huokoa." "yule anayeniokoa"