sw_tn/psa/018/035.md

16 lines
692 B
Markdown

# ngao ya wokovu wako
Hapa mwandishi anazungumzia ulinzi wa Mungu kana kwamba ni ngao. Nomino dhahania ya "wokovu" inaweza kuelezwa kama kitenzi "okoa." "ulinzi wako na kuniokoa"
# Mkono wako wa kuume ... fadhili zako
Zote hizi ni njia zingine za kumwakilisha Mungu mwenyewe.
# sehemu pana kwa ajili ya miguu yangu chini yangu
Mwandishi anazungumzia ulinzi ambao Mungu ameutoa kana kwamba ni eneo pana kwa ajili yake kusimama. "sehemu salama kwa ajili yangu"
# miguu yangu haijateleza
Hapa "miguu yangu" inamaanisha mtu mwenyewe. Mwandishi anazungumzia usalama wa ulinzi wa Mungu kana kwamba alikuwa akisimama mahali ambapo hawezi kuteleza wala kuanguka. "Sijateleza" au "Niko salama"