sw_tn/psa/018/022.md

28 lines
675 B
Markdown

# Kwa amri zake zote za haki ... sijazigeuka
Vishazi hivi viwili vina maana ya kufanana. Mwandishi anarudia mawazo haya kwa ajili ya mkazo.
# zimekuwa mbele yangu
"zimeniongoza" au "nimezikumbuka"
# Pia nimekuwa bila hatia ... nimejitenga na dhambi
Vishazi hivi viwili vina maana ya kufanana. Mwandishi anarudia mawazo haya kwa ajili ya mkazo.
# bila hatia mbele yake
"bila hatia kulingana na yeye"
# nimejitenga na dhambi
"sijatenda dhambi"
# mikono yangu ilikuwa misafi
Kuwa na "mikono misafi" inamaanisha kuwa mtu hana hatia na kosa. "matendo yangu yote yalikuwa sawa"
# mbele ya macho yake
Hii inamaanisha uwepo wa Mungu. "mbele yake" au "kulingana na yeye"