sw_tn/psa/011/001.md

28 lines
841 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Kwa mwanamuziki mkuu
"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"
# Zaburi ya Daudi
Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.
# ninamkimbilia Yahwe
Kwenda kwa Yahwe kwa ajili ya ulinzi kunazungumziwa kama kumkimbilia. "kwenda kwa Yahwe kwa ulinzi"
# utasemaje kwangu, "Kimbia kama ndege milimani?"
Swali hili linaulizwa kutoa msisitizo. Linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Kwa hiyo usiniambie kukimbia!"
# Maana tazama! Waovu wanaanda upinde wao. Wanafanya tayari mishale yao kwenye nyuzi kupiga gizani kwa wanyofu moyoni.
"Tazama! waovu wanajiandaa kuvamia watu wanyofu"
# wanyofu moyoni
Hapa "wanyofu moyoni" inamaanisha watu wanaomcha Mungu au wenye haki.