sw_tn/mrk/14/intro.md

1.2 KiB

Marko 14 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huweka kila mstari wa mashairi kwa upande wa kulia zaidi kuliko maandiko yote ili iwe rahisi kusoma. ULB inafanya hivyo kwa mashairi katika 14:27,62, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Kula mwili na damu

Marko 14:22-25 inaelezea chakula cha mwisho cha Yesu na wafuasi wake. Wakati huu, Yesu aliwaambia kwamba kile walichokuwa wakila na kunywa kilikuwa mwili wake na damu yake. Karibu makanisa yote ya kikristo huadhimisha "Meza ya Bwana," "Ekaristi", au "Mkutano wa Kikawa" kukumbuka chakula hiki.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Abba, Baba

"Abba" ni neno la Kiaramu ambalo Wayahudi walitumia kuzungumza na baba zao. Marko analiandika kama linavyotamkwa na kisha kulifasiri. (See: rc://*/ta/man/translate/translate-transliterate)

"Mwana wa Mwanadamu"

Yesu anajiita mwenyewe "Mwana wa Binadamu" katika sura hii (Marko 14:20). Lugha yako huenda haiwezi kuwaruhusu watu kujizungumzia wenyewe kana kwamba wanaongea juu ya mtu mwingine. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/sonofman]] and [[rc:///ta/man/translate/figs-123person]])

<< | >>