sw_tn/luk/22/33.md

717 B

Jogoo hatawika leo, kabla hujanikana mara tatu kwamba unanijua

Mpangilio wa maneno unaweza kubadilishwa na kusomeka: "Utanikana mara tatu kwamba unanijua kabla jogoo hajawika siku hii ya leo"

Jogoo hatawika leo, kabla hujanikana

Hii inaweza kuongelewa kwa namna chanya: "Jogoo atawika siku hii ya leo mara tu baada ya kunikana."

Jogoo hatawika

Hapa, kuwika kwa Jogoo kunaonyesha muda fulani katika siku. Jogoo mara nyingi huwika kabla ya jua kuchomoza asubuhi.

siku hii

Siku ya Kiyahudi huanza wakati wa kuzama kwa jua. Yesu alikuwa anaongea baada ya jua kuwa limezama. Jogoo angeliwika muda mchache kabla ya asubuhi. Asubuhi ilikuwa sehemu ya "siku hii." Tafsiri mbadala: "Usiku wa leo" au "asubuhi."