sw_tn/luk/22/33.md

16 lines
717 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Jogoo hatawika leo, kabla hujanikana mara tatu kwamba unanijua
Mpangilio wa maneno unaweza kubadilishwa na kusomeka: "Utanikana mara tatu kwamba unanijua kabla jogoo hajawika siku hii ya leo"
# Jogoo hatawika leo, kabla hujanikana
Hii inaweza kuongelewa kwa namna chanya: "Jogoo atawika siku hii ya leo mara tu baada ya kunikana."
# Jogoo hatawika
Hapa, kuwika kwa Jogoo kunaonyesha muda fulani katika siku. Jogoo mara nyingi huwika kabla ya jua kuchomoza asubuhi.
# siku hii
Siku ya Kiyahudi huanza wakati wa kuzama kwa jua. Yesu alikuwa anaongea baada ya jua kuwa limezama. Jogoo angeliwika muda mchache kabla ya asubuhi. Asubuhi ilikuwa sehemu ya "siku hii." Tafsiri mbadala: "Usiku wa leo" au "asubuhi."