sw_tn/luk/22/01.md

1.0 KiB

Maelezo ya ujumla:

Hii ni sehemu inayofuata ya simulizi. Yuda anakubali kumsaliti Yesu. Mistari hii inatupa taarifa za msingi kuhusu sehemu hii ya simulizi.

Basi

Neno hili linatumika hapa sehemu mpya ya simulizi

sikukuu ya mkate usiyotiwa chachu

sikukuu hii ilikuwa inaitwa kwa jina hili kwa sababu wakati wa sikukuu, Wayahudi hawakula mkate ambao ulikuwa umetengenezwa na chachu. Tafsiri mbadala: "Sikukuu ambapo wangekula mkate usiyotiwa chachu"

Mkate usiyotiwa chachu

Huu ni mkate ambao hauna chachu au hamila ili kuufanya uumuke. Tafsiri mbadala: "Mkate bila Hamila."

ilikuwa imekaribia

"ilikuwa tayari sana kuanza"

namna ya kumuua Yesu

Makuhani na waandishi hawakuwa na mamlaka ya kumuua Yesu wao wenyewe, lakini walitegemea kupata watu wengine wa kumuua. Tafsiri mbadala: "Namna gani ambavyo wangesababisha Yesu kuuwawa" au "namna ambavyo wangesababisha mtu amuuwe Yesu."

waliwaogopa watu

Inaweza kutafsiriwa kama 1) "walikuwa na wasiwasi wa kile ambacho watu wangefanya" au 2) "walikuwa na wasiwasi kwamba watu wangemfanya Yesu mfalme."