# Maelezo ya ujumla: Hii ni sehemu inayofuata ya simulizi. Yuda anakubali kumsaliti Yesu. Mistari hii inatupa taarifa za msingi kuhusu sehemu hii ya simulizi. # Basi Neno hili linatumika hapa sehemu mpya ya simulizi # sikukuu ya mkate usiyotiwa chachu sikukuu hii ilikuwa inaitwa kwa jina hili kwa sababu wakati wa sikukuu, Wayahudi hawakula mkate ambao ulikuwa umetengenezwa na chachu. Tafsiri mbadala: "Sikukuu ambapo wangekula mkate usiyotiwa chachu" # Mkate usiyotiwa chachu Huu ni mkate ambao hauna chachu au hamila ili kuufanya uumuke. Tafsiri mbadala: "Mkate bila Hamila." # ilikuwa imekaribia "ilikuwa tayari sana kuanza" # namna ya kumuua Yesu Makuhani na waandishi hawakuwa na mamlaka ya kumuua Yesu wao wenyewe, lakini walitegemea kupata watu wengine wa kumuua. Tafsiri mbadala: "Namna gani ambavyo wangesababisha Yesu kuuwawa" au "namna ambavyo wangesababisha mtu amuuwe Yesu." # waliwaogopa watu Inaweza kutafsiriwa kama 1) "walikuwa na wasiwasi wa kile ambacho watu wangefanya" au 2) "walikuwa na wasiwasi kwamba watu wangemfanya Yesu mfalme."