sw_tn/luk/09/intro.md

2.6 KiB

Luka 09 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Kuhubiri ufalme wa Mungu"

Kuna mzozo kati ya wasomi kuhusu maana ya ufalme we Mungu hapa unamaanisha utawala wa Mungu duniani au ujumbe wa injili (Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi za mwanadamu). Ni bora kutafsiri hii kama "kuhubiri juu ya ufalme wa Mungu" au "kuwafundisha kuhusu jinsi Mungu angeweza kujionyesha kuwa mfalme." "Ni bora usitafsiri maneno hayo kama mfano wa injili kwa sababu haifai hapa. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-metaphor)

Eliya

Nabii Malaki alitabiri kwamba siku moja Eliya angerudi kabla Masihi hajaja. Yesu anaelezea kwamba Yohana Mbatizaji alitimiza unabii huu kwa kumtumikia Mungu kwa namna ileile kama Eliya. Eliya ametajwa kwa njia mbili tofauti katika sura hii, kama mtu halisi na kurudi kimfano kwa Eliya. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/prophet]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/christ]])

"Ufalme wa Mungu"

Maneno 'ufalme wa Mungu' katika sura hii yalitumikiwa kwa kutaja ufalme utakapokuja wakati maneno haya yaliyosemwa. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/kingdomofgod)

"Waliona utukufu [wa Yesu]"

Katika Maandiko utukufu wa Mungu unaonekana kama mwanga wa kunga'a sana. Utukufu wa Mungu Katika Maandiko utukufu wa Mungu unaonekana kama mwanga wa kunga'a sana kwa mtu anayeuona. Tukio hilo, iliyoandikwa katika sura hii, linaitwa "kugeuka sura," asababu Yesu aligeuka sura na kubadilika sura ili aonyeshe utukufu wake wa kiungu. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/glory]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/fear]])

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kitendawili

Kitendawili ni taarifa inayoonekana kuwa ya ajabu, ambayo ni kana kwamba inajikana yenyewe, lakini kwa hakika sio ya ajabu. Mfano wa kitendawili katika sura hii: "Yeyote anayetaka kuokoa maisha yake ataipoteza, na yeyote anayepoteza maisha yake kwa ajili yangu ataipata." (Luka 9:24).

"Mwana wa Binadamu"

Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu." Lugha zingine haziwezi kuruhusu mtu kujitaja mwenyewe kama 'mtu wa tatu.' (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/sonofman)

"Kupokea"

ULB inatumia neno hili mara kadhaa katika sura hii kwa maana mbalimbali. Yesu anasema, "Yeyote akipokea mtoto mdogo kama huyu kwa jina langu, yeye ananipokea pia, na yeyote akinipokea mimi, anapokea pia yeye aliyenituma" (Luka 9:48). Katika aya hii, "kupokea" inaweza kutafsiriwa kama "kutumikia." Katika mstari mwingine inasemwa, "watu huko hawakumpokea" (Luka 9:53). Katika aya hii, "kupokea" inaweza kutafsiriwa kama "kuamini" au "kukubali." (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/believe)

<< | >>