sw_tn/luk/02/45.md

841 B

ikatokea kwamba

Kauli hii ilitumika hapa kuashiria umhimu wa tukio katika simulizi. Kama lugha yako ina namna ya kufanya hivi, ufikiri kuitumia hapa.

katika hekalu

Hii inarejea kwenye kiwanja cha hekalu. Makuhani tu walioruhusiwa ndani ya hekalu. NI: "katika kiwanja cha hekalu" au "kwenye hekalu."

katikati ya

Hii haina maana ya katikati kabisa. Zaidi, inamaanisha, "kati" au "pamoja na" au "kuzunguka."

waalimu

"waalimu wa dini" au "wale ambao waliwafundisha watu kuhusu Mungu"

wote waliosikia walishangaa

Walikuwa hawawezi kuelewa namna gani mvulana wa miaka kumi na miwili asiye na elimu ya dini ajibu vizuri hivyo.

kwenye ufahamu wake

"kwa kiwango kipi alielewa" au "kwamba yeye anaelewa mengi sana kuhusu Mungu"

majibu yake

"kwa namna alivyo wajibu vizuri" au "kwamba yeye aliwajibu maswali yao vizuri sana"