sw_tn/luk/01/34.md

1.1 KiB

Namna gani hili litatokea

NI: "Hili linawezekana kwa namna gani?" Ingawa Mariamu hakuelewa jinsi itakavyotokea, yeye hakuwa na shaka kwamba ingelitokea.

Mimi sijalala pamoja na mwanaume yeyote

Mariamu alitumia hali halisi kusema kwamba hajawahi kuhusika kwenye tendo la ngono. NI: "Mimi ni bikra" (UDB)

Roho Mtakatifu atakuja juu yako

utungaji mimba wa Mariamu ungelianza na ujio wa Roho Mtakatifu kwake.

atakuja juu

"kuja ghafla" au "atakutokea"

nguvu ya aliye Juu Sana

Ilikuwa ni nguvu ya Mungu ingelikuja zaidi ya kawaida kumsababisha Mariamu kuwa mjamzito hata wakati akiwa bado akabaki bikra. Hakikisha hii haidokezi hali au muungano wa ngono - huu ulikuwa muujiza.

itakuja juu yako

"utafunikwa kma kivuli"

mtakatifu

"mtoto mtakafu" au "mtoto mchanga mtakatifu"

atakuwa akiitwa

Maana zinazowezekana 1)"watu watamwita" au 2) Mungu atamwita

Hivyo mtakatifu atakayezaliwa ataitwa Mwana wa Mungu

Ingawaje mama yake Yesu alikuwa mwanadamu, Mungu zaidi ya kawaida alimweka Yesu tumboni mwake. Hivyo basi, Mungu alikuwa Baba yake, na Yesu alikuwa anaitwa "Mwana wa Mungu."

Mwana wa Mungu

Hii ni sifa mhimu kwaajili ya Yesu.