sw_tn/luk/01/30.md

1.1 KiB

Usiwe na hofu, Mariamu

Malaika hakutaka Mariamu kuwa na woga kwa ujio wake, kwasababu Mungu alimtuma ujumbe mzuri.

umepata wema wa Mungu

Nahau "kupata fadhila" inamaana kupokelewa vizuri na mtu fulani. Sentensi inaweza kugeuzwa kuonesha Mungu kama mtenda. NI: "Mungu ameamua kutoa neema yake" au "Mungu anaonesha wema wake."

utakuwa na ujauzito tumboni mwako na kuzaa mwana ... Yesu ... Mwana wa aliye Juu Sana

Mariamu atazaa "mwana" atakayeitwa "Mtoto wa aliye Juu Sana" (UDB). Yesu ni mtoto aliyezaliwa na mama mwanadamu, na Yeye vilevile ni Mwana wa Mungu. Maneno haya yatafsiriwe kwa uanglifu sana.

ataitwa

Maana zinazowezekana ni 1) "watu watamwita" au 2) "Mungu atamwita."

Mwana wa aliye Juu Sana

Hii ni sifa mhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.

Kupewa kiti cha mhenga wake Daudi

Kiti kinawakilisha mamlaka ya mfalme kutawala. NI: "kumpa mamlaka kutawala kama mfalme kama baba yake Daudi alivyofanya"

hapatakuwa na mwisho kwa ufalme wake

Kauli hasi ""hakuna mwisho" sisitiza kwamba utaendelea milele. Pia inaweza kusemwa kwa kauli chanya. NI: "ufalme wake hautaisha."