sw_tn/luk/01/21.md

972 B

Sasa

Hii inadokeza kuhama katika simulizi kutokana nakilichotokea ndani ya hekalu kwenda kilichotokea nje. NI: "Wakati huo" au "Wakati malaika na Zakaria wanazungumza."

Walitambua kwamba alishapata maono wakati akiwa hekaluni. Aliendelea kuwafanyia ishara na alibaki kimya.

Mambo haya huenda yalitokea muda uleule, na ishara za Zakaria ziliwasaidia watu kuelewa kwamba amepata maono. Inaweza ikawa msaada kwa wasikilizaji wako wabadili utaratibu kuonesha hivyo. NI: "Yeye aliendelea kuwafanyia ishara na alibaki kimya. Hivyo walitambua kwamba alipata maono wakati akiwa ndani ya hekalu."

maono

maelezo yaliyotangulia yanaashiria kwamba Gabrieli alikuja kweli kwa zakaria hekaluni. Watu, hawajui hilo, walidhani Zakaria aliona maono.

ilitokea

Kauli hii inahamisha simulizi kwenda mbele ambapo huduma ya Zakaria ilikuwa inaishia.

alikwenda nyumbani kwake

Zakaria alikuwa haishi Yerusalemu, ambapo palikuwa na hekalu. Alisafiri kwenda kwenye mji alioishi.