sw_tn/luk/01/08.md

1.1 KiB

Sasa ikaja kuwa

Hii kauli ilitumika kubadili simulizi kutoka taarifa za mwanzo kwenda kwa wahusika.

katika utaratibu wa mgawo wake

"ilipokuwa zamu ya kundi lake" au "wakati ulipowadia wa kundi lake kuhudumu"

kutokana na desturi ya kuchagua kuhani yupi ambaye ... achome ubani

Sentensi hii inatupa sisi taarifa kuhusu wajibu wa kikuhani.

taratibu za kidesturi

"mfumo wa kiutamaduni" au "njia yao ya kawaida"

kuchagua kwa kura

kura ilikuwa ni jiwe lenye alama ambalo lilitupwa au viringishwa chini ili kwamba liwasaidie kuamua jambo fulani. Makuhani waliamini kwamba Mungu aliielekeza kura kuwaonesha kile walichokitaka makuhani kuchagua.

hivyo anaweza kuchoma ubani

Makuhani walikuwa wanachoma harufu nzuri kama sadaka kwa Mungu kila asubuhi na jioni katika madhabahu maalumu ndani ya hekalu.

mkutano wote wa watu

"Idadi kubwa ya watu" au "Watu wengi"

nje

Kiwanja ilikuwa ni eneo linalolizunguka hekalu. NI: "nje ya jengo la hekalu" au "kwenye kiwanja nje ya hekalu."

katika wakati

"kwenye muda uliopangwa." Haikowazi kama ilikuwa muda wa asubuhi au jioni kwaajili ya sadaka ya ubani.