sw_tn/luk/01/08.md

36 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Sasa ikaja kuwa
Hii kauli ilitumika kubadili simulizi kutoka taarifa za mwanzo kwenda kwa wahusika.
# katika utaratibu wa mgawo wake
"ilipokuwa zamu ya kundi lake" au "wakati ulipowadia wa kundi lake kuhudumu"
# kutokana na desturi ya kuchagua kuhani yupi ambaye ... achome ubani
Sentensi hii inatupa sisi taarifa kuhusu wajibu wa kikuhani.
# taratibu za kidesturi
"mfumo wa kiutamaduni" au "njia yao ya kawaida"
# kuchagua kwa kura
kura ilikuwa ni jiwe lenye alama ambalo lilitupwa au viringishwa chini ili kwamba liwasaidie kuamua jambo fulani. Makuhani waliamini kwamba Mungu aliielekeza kura kuwaonesha kile walichokitaka makuhani kuchagua.
# hivyo anaweza kuchoma ubani
Makuhani walikuwa wanachoma harufu nzuri kama sadaka kwa Mungu kila asubuhi na jioni katika madhabahu maalumu ndani ya hekalu.
# mkutano wote wa watu
"Idadi kubwa ya watu" au "Watu wengi"
# nje
Kiwanja ilikuwa ni eneo linalolizunguka hekalu. NI: "nje ya jengo la hekalu" au "kwenye kiwanja nje ya hekalu."
# katika wakati
"kwenye muda uliopangwa." Haikowazi kama ilikuwa muda wa asubuhi au jioni kwaajili ya sadaka ya ubani.