sw_tn/lev/18/01.md

7.3 KiB

Yahweh

Hili ni jina Mungu ambalo alimwambia Musa kwenye kicha kilichowaka moto. Mungu alisema kwamba hili ndilo lilikuwa jina lake milele.

Musa

Musa alikuwa nabii na kiongozi wa watu wa Waisraeli kwa zaidi ya miaka 40.

Alipokuwa mtoto, wazazi wake Musa, walimweka yeye kwenye kikapu cha mianzi ya Mto Nile ili kumficha kwa Farao wa Misri. Dada yake Miriamu dada yake Musa, Alimwangalia yeye huko. Maisha ya Musa yaliokolewa tu binti alipomwona na kumchukua kwenda naye Ikulu ili kumlea kama mwanae.

Mungu alimchagua Musa kuwaweka huru Waisraeli kutoka utumwani Misri na kuwaongoza kwenda katika Nchi ya Ahadi.

Baada ya kutoka kwa Waisraeli Misri na walipokuwa wangali wakizunguka jangwani, Mungu alimpa Musa mbao mbili za mawe zilioandikwa Amri Kumi juu yake.

Karibu kabisa na mwisho wa maisha yake, Musa aliiona tu Nchi ya Ahadi, lakini haingia kuishi humo kwa sababu hakumtii Mungu.

Kikundi cha watu, watu, watu wa,

Ule usemi "watu" au "vikundi vya watu" humaanisha vikundi vya watu wanaoshiriki lugha na utamaduni mmoja. Kile kirai "watu wa" mara kwa mara humaanisha kusanyanika la watu katika eneo fulani au katika tukio maalum.

Mungu anapotenga "kikundi cha watu" kwa ajili yake, humaanisha alichagua watu fulani ili wawe wake na kumtumikia yeye.

Katika nyakiti za Biblia, washirika wa kikundi cha watu kwa kawaida walikuwa na wazazi au mababu wamoja na waliishi mahali pamoja katika taifa au eneo maalum la nchi.

Kwa utegemeana na muktadha, kirai kama vile "watu wako" chaweza kumaanisaha "kikundi cha watu wako" au "famikia yako" au "jamaa zako."

Ule usemo "watu" mara kwa mara limetumika kumaanisha vikundi vyote vya watu juu ya nchi." Wakati mwingine zaidi lilimaanisha hasa kwa watu wasio Waisraeli au wasiomtumikia Yahweh. Katika tafasiri zingine za kiingereza ule msemo "mataifa" pia umetumika katika njia hii.

MAPENDAKEZO YA UFASIRI. Ule msemo "kikundi cha watu" waweza kufasiriwa kwa neno au kirai chenye kumaanisha, "kundi kubwa la kifamilia" au "ukoo" au "kikundi cha kikabila."

Kirai kama vile "watu wangu" chaweza kufasiriwa kama "jamaa zangu" au "Waisraeli wenzangu" au "familia yangu" au "watu wa kikundi changu," kutegemeana na muktadha.

Yale maelezo "nitawatawanya miongoni mwa watu" pia yaweza kufasiriwa "nitasababisha kwenda na kuishi pamoja na vikundi mbali mbali vya watu wengi" au "sababisha kutengana ninyi kwa ninyi na kwenda kuishi katika mikoa mingi tofauti ya ulimwengu.

Ule msemo "watu" waweza kufasiriwa "watu ulimwenguni" au "vikundi vya watu," kutegemeana na muktadha.

Kile kirai "watu wa" chaweza kufasiriw kama, "kila mmoja aishie katika" au "watu wa kutoka uzao wa" au "familia ya," kutegeana na ama linafuatiwa na jina la mahali au mtu.

"watu wote wa ulimwengu" yaweza kufasiriwa kama, "kila nafsi ulimwenguni" au "watu wote."

Kile kirai "watu" pia chaweza kufasiriwa kama "kikundi cha watu" au "watu fulani" au "kikundi cha watu" au "jamii ya watu" au "familia ya watu"

Israeli, Waisraeli, taifa la Israeli

Ule msemo "Israeli" ni jina ambalo Mungu alimpa Yakobo. Humaanisha, "yeye hushindana na Mungu."

Wazao wa Yakobo walikuja kujulikana kama "watu wa Israeli," "taifa la Israeli," au "Wasraeli." Taifa la Israeli

Mungu alitengeneza agano lake watu wa Israeli. Walikuwa watu wake wateule.

Taifa la Israeli liliundwa na makabila kumi na mbili.

Mara tu baada ya kufa kwa mfalme Sulemani, Isrseli iligawanyika katika falme mbili: Ufalme wa kusuni, uliitwa "Yuda" na ule ufalme wa kaskazini ukaitwa "Israeli."

Mara kwa mara ule msemo "Israeli" waweza kufasiriliwa kama, "watu wa Israeli" au "taifa la Israeli," kwa kutegemeana na muktatha.

Mungu

Kwenye Biblia Neno "Mungu" humaanisha nafsi ya milele aliyeumba ulimwengu pasipo kitu. Mungu huishi kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. jina binafsi la Mungu ni "Yahweh" . Siku zote Mungu alikuwapo; alikuwapo kabla ya kabla ya kitu chochote kuwapo. Naye ataendelea kuwako milele

. Yeye ndiye Mungu wa kweli na ana mamlaka juu ya vitu vyote hulimwenguni.

. Mungu ni mwenye haki kwa ukamilifu, ni mwenye hakima pasipo na kikomo, mtakatifu, bila dhambi, mwenye haki, rehema, na upendo.

. Yeye ni Mungu atunzaye agano, ambaye hutimiza ahadi zake.

. Watu waliumbwa ili wamwambudu Mungu naye ndiye Yeye pekee imewapasa wao kumwabudu.

. Mungu lilifunua jina lake kuwa ni "Yahweh" ambalo humaanisha, " yeye ndiye" au "Mimi ndimi" au "Yule aliyopo (siku zote)"

. Pia Biblia hufundisha juu ya "miungu ya uongo" ambayoo ni sanamu zisizo na uhai ambayo watu huiabudu kimakosa.

MAPENDEKEZO YA UFASIRI

. Njia za kufasiri "Mungu zingejumuisha maneno kama "Uungu" au "Muumba" au "Mwenye Mamlaka yote"

. Njia zingine za kufasiri "Mungu" zaweza kuwa, "Muumbaji wa vyote" au "Bwana Mwenye mamlaka isiyo na mipaka" au "Mwenye Mamlaka yote milele."

Zingatia jinsi Mungu anavyotajwa katika lugha ya kieneo au kitaifa. Yawezekana kuwa tayari lipo neno kuhusu "Mungu" katika lugha inayotafsiriwa. Kama ndivyo, ni muhimu kuhakikisha kwamba neno hili linafaa kwa sifa baishi za Mungu wa kweli kama anavyoelezwa hapo juu.

Lugha nyingi huanza na herifu kubwa ya neno kwa Mungu aliye wa kweli ili kulitofautisha na neno kwa mungu wa uongo.

Njia nyingine ya kuonesha tofauti hizi ingetumika misemo miwili tofauti kwa "Mungu" na "muungu"

Kile kirai, "nitakuwa Mungu wao nao watakuwa atu wangu" pia chaweza kufasiriwa kama, "Mimi, Mungu, nitatawala juu ya watu nao wataniabudu mimi."

Misri, Mmisri

Misri ni taifa lililoko upande wa kaskazini mashariki mwa Africa, kusini magharibi mwa nchi ya Kanaani. Mmisri ni mtu anayetoka katika nchi ya Misri.

. Zamani za kale, Misri lilikuwa taifa lenye nguvu na tajiri.

. Misri ya zamani iligawanyika katika sehemu mbili, Misri ya chini (sehemu ya kaskazini mahali ambapo mto Nile ulitiririka kuelekea Baharini) na Misri ya juu (sehemu ya kusini). Katika Agano la Kale, sehamu hizi zilitajwa kama "Misri" na "Pathrosi" katika lugha ya asili.

Mara nyingi kilipokosekana chakula huko Kanaani, mababa wa Israeli walisafiri kwenda Misri ili kununua chakula kwa ajili aya familia zao.

Kwa muda wa mamia ya miaka, Waisraeli walikuwa watumwa huko Misri.

Yusufu na Mariamu waliterekia Misri pamoja na mtoto mchanga Yesu ili kumtoroka Herode Mkuu.

Maisha, ishi, kuishi, -wa mzima

Misemo hii yote humaanisha kuwa mzima kimaumbile, siyo mfu. Pia yametuka kiishara kumaanisha kuwa hai kiroho. Ifuatayo inazungumzia inavyomaanisha kuwa na "uhai wa kimwili" na "Uhai wa Kiroho"

MAPENDEKEZO YA UFASIRI

. Kwa utegemeana na muktadha, "maisha yaweza kufasiriwa kama "uwepo" au "nafsi" au "moyo" au "aishie" au "uzoefu"

. Ule msemo "ishi" waweza kufasiriwa "kaa" au "kuwepo."

Yale amelezo "mwisho wa maisha" yangeweza kufasiriwa kama, "alipokoma kuishi."

Yale maelezo "alitunza uhai wao" yangeweza kufasiriwa kama, "aliwaruhusu kuishi" au "hakuwaua wao."

Ule usemi "walihatarisha maisha yao" ungeweza kufasiriwa kama, "walijiweka wenyewe hatarini" au walifanya jambo fulani ambalo lingekuwa limishawaua wao."

Kifungu cha Biblia kinapozungumzia kuwa hai kiroho, "uhai"pia ungefasiriwa kama, "maisha ya kiroho" au "Uzima wa milele" kutegemeana na muktatha"

Wazo la "maisha ya kiroho" lingeweza kufasiriwa pia kama "Mungu anatufanya hai katika roho zetu" au "maisha mpya yatolewayo na Roho wa Mungu" au "kufanywa hai katika utu wetu wa ndani."

Kwa kutegemeana na muktatha, neno "-pa maisha" laweza pia kufasiriwa kama "sababisha kuwa hai" au -pa maisha mapya" au "sababisha kuishi milele."