Alipokuwa mtoto, wazazi wake Musa, walimweka yeye kwenye kikapu cha mianzi ya Mto Nile ili kumficha kwa Farao wa Misri. Dada yake Miriamu dada yake Musa, Alimwangalia yeye huko. Maisha ya Musa yaliokolewa tu binti alipomwona na kumchukua kwenda naye Ikulu ili kumlea kama mwanae.
Ule usemi "watu" au "vikundi vya watu" humaanisha vikundi vya watu wanaoshiriki lugha na utamaduni mmoja. Kile kirai "watu wa" mara kwa mara humaanisha kusanyanika la watu katika eneo fulani au katika tukio maalum.
Mungu anapotenga "kikundi cha watu" kwa ajili yake, humaanisha alichagua watu fulani ili wawe wake na kumtumikia yeye.
Katika nyakiti za Biblia, washirika wa kikundi cha watu kwa kawaida walikuwa na wazazi au mababu wamoja na waliishi mahali pamoja katika taifa au eneo maalum la nchi.
Ule usemo "watu" mara kwa mara limetumika kumaanisha vikundi vyote vya watu juu ya nchi." Wakati mwingine zaidi lilimaanisha hasa kwa watu wasio Waisraeli au wasiomtumikia Yahweh. Katika tafasiri zingine za kiingereza ule msemo "mataifa" pia umetumika katika njia hii.
Kirai kama vile "watu wangu" chaweza kufasiriwa kama "jamaa zangu" au "Waisraeli wenzangu" au "familia yangu" au "watu wa kikundi changu," kutegemeana na muktadha.
Yale maelezo "nitawatawanya miongoni mwa watu" pia yaweza kufasiriwa "nitasababisha kwenda na kuishi pamoja na vikundi mbali mbali vya watu wengi" au "sababisha kutengana ninyi kwa ninyi na kwenda kuishi katika mikoa mingi tofauti ya ulimwengu.
Kile kirai "watu wa" chaweza kufasiriw kama, "kila mmoja aishie katika" au "watu wa kutoka uzao wa" au "familia ya," kutegeana na ama linafuatiwa na jina la mahali au mtu.
Mara tu baada ya kufa kwa mfalme Sulemani, Isrseli iligawanyika katika falme mbili: Ufalme wa kusuni, uliitwa "Yuda" na ule ufalme wa kaskazini ukaitwa "Israeli."
Mara kwa mara ule msemo "Israeli" waweza kufasiriliwa kama, "watu wa Israeli" au "taifa la Israeli," kwa kutegemeana na muktatha.
# Mungu
Kwenye Biblia Neno "Mungu" humaanisha nafsi ya milele aliyeumba ulimwengu pasipo kitu. Mungu huishi kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. jina binafsi la Mungu ni "Yahweh"
. Njia zingine za kufasiri "Mungu" zaweza kuwa, "Muumbaji wa vyote" au "Bwana Mwenye mamlaka isiyo na mipaka" au "Mwenye Mamlaka yote milele."
Zingatia jinsi Mungu anavyotajwa katika lugha ya kieneo au kitaifa. Yawezekana kuwa tayari lipo neno kuhusu "Mungu" katika lugha inayotafsiriwa. Kama ndivyo, ni muhimu kuhakikisha kwamba neno hili linafaa kwa sifa baishi za Mungu wa kweli kama anavyoelezwa hapo juu.
Lugha nyingi huanza na herifu kubwa ya neno kwa Mungu aliye wa kweli ili kulitofautisha na neno kwa mungu wa uongo.
Njia nyingine ya kuonesha tofauti hizi ingetumika misemo miwili tofauti kwa "Mungu" na "muungu"
Kile kirai, "nitakuwa Mungu wao nao watakuwa atu wangu" pia chaweza kufasiriwa kama, "Mimi, Mungu, nitatawala juu ya watu nao wataniabudu mimi."
# Misri, Mmisri
Misri ni taifa lililoko upande wa kaskazini mashariki mwa Africa, kusini magharibi mwa nchi ya Kanaani. Mmisri ni mtu anayetoka katika nchi ya Misri.
. Zamani za kale, Misri lilikuwa taifa lenye nguvu na tajiri.
. Misri ya zamani iligawanyika katika sehemu mbili, Misri ya chini (sehemu ya kaskazini mahali ambapo mto Nile ulitiririka kuelekea Baharini) na Misri ya juu (sehemu ya kusini). Katika Agano la Kale, sehamu hizi zilitajwa kama "Misri" na "Pathrosi" katika lugha ya asili.
Misemo hii yote humaanisha kuwa mzima kimaumbile, siyo mfu. Pia yametuka kiishara kumaanisha kuwa hai kiroho. Ifuatayo inazungumzia inavyomaanisha kuwa na "uhai wa kimwili" na "Uhai wa Kiroho"
Ule usemi "walihatarisha maisha yao" ungeweza kufasiriwa kama, "walijiweka wenyewe hatarini" au walifanya jambo fulani ambalo lingekuwa limishawaua wao."
Wazo la "maisha ya kiroho" lingeweza kufasiriwa pia kama "Mungu anatufanya hai katika roho zetu" au "maisha mpya yatolewayo na Roho wa Mungu" au "kufanywa hai katika utu wetu wa ndani."