sw_tn/lev/17/10.md

737 B

Nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo

Neno "uso" huwakilisha nafsi. Nahu hii humaanisha kumkataa mtu au kitu fulani. : "Nitakuwa nyume na mtu huyo" au "nitamkataa mtu huyo" au "Nitamkataa huyu mtu"

kumkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake

Mtu aliyeondolewa kwenye jamii yake anazungumziwa kana kwamba amekatwa kwa watu wake, kama mtu akatavyo tawi kutoka kwenye mti. : "Sitamruhusu mtu huyu aendelee kuishi miongoni mwa watu wake tena"au "Nitamtenga mtu huyo kutoka kwa watu wake"

Kwa kuwa uhai wa mnyama yeyote umo katika damu yake...ipatanishayo kwa ajili ya uhai

Hii humaanisha MUngu huitumia damu kupatanisha kwa ajili ya dhambi za watu kwa sababu damu ni uhai. Watu wasinywe damu kwa sanbabu ina kusudi hili maalum.