sw_tn/lev/07/19.md

1015 B

9Nyama yoyote igusayo kitu kilicho najisi haitaliwa

Hii yaweza kufasiriwa katika mtindo wa utendaji. : "Hakuna awezaye kula nyama inayogusa kitu fulani kilichonajisi"

kitu kilicho najisi

Kitu fulani ambacho Yahweh amekitamka kuwa hakifai kukigusa au kukila kinasungumziwa kana kwamba kilikuwa najisi kimaumbile.

Ni lazima iteketezwe kwa moto

Hii yaweza kufasiriwa katika mtindo wa utendaji. : "yapasa uiteketeze kwa moto"

yeyote aliye safi

Mtu mwenye kukubalika kwa kusudi la Mungu anazungumziwa kana kwamba ni mtu aliyekuwa safi kimaumbile.

mtu yeyote aliyenajisi

Mtu asiyekukubalika kwa kusudi la Mungu anazungumziwa kana kwamba ni mtu aliyekuwa mchafu kimaumbile.

yapasa mtu huyu akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.

Mtu anayetengwa kutoka kwa jamii yake anazungumziwa kana kwamba amkwisha kukatwa kutoka kwa watu wake, kama vile mtu akatavyo kipande cha nguo au tawi kutoka kwenye mti. : "mtu huyo hawezi kuishi miongoni mwa watu wake" au "yapasa umtenge mtu huyo kutoka kwa watu wake"