sw_tn/jhn/05/01.md

919 B

Maneno kwa Ujumla:

hili ni tukio linalofuata katika simulizi,ambalo Yesu anapanda kwenda Yerusalemu na anamponya mtu.Mistari hii inatoa mambo ya nyuma kuhusu mwanzoni mwa simulizi.

Baada ya hili

ina maanisha baada Yesu kumponya mwana wa afisa. ona namna ambavo unaweza kufasiri hili.

kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi

"Wayahudi walikuwa wakisherehekea sikukuu"

alipanda kwenda Yerusalemu

Yerusalemu iko juu ya kilima. Mabarabara ya Yerusalemu yalipanda juu na kutelemka katika vilima vidogo . Kama lugha yako ina neno tofauti kwa kupanda juu ya kilima kuliko kuliko kutembea katika tambarare unaweza kuitumia hapa.

dimbwi

hili lilikuwa ni shimo chini ambalo watu walijaza maji. Wakati mwingine walilizungushia kwa vigae na mawe.

Bethzatha

"Bethzatha" maana yake ni nyumba ya huruma.

matao

muundo ulioezekwa angalau pasipo kuwa ukuta mwingine katika jengo.

Idadi kubwa ya watu

"watu wengi"