sw_tn/jhn/04/intro.md

2.6 KiB

Yohana 04 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Yohana 4:4-38 ni habari moja inayozingatia mafundisho ya Yesu kama "maji yaliyo hai," anayewapa wote wanaomwamini uzima wa milele. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/believe)

Dhana maalum katika sura hii

"Ilikuwa ni lazima yeye apitie Samaria"

Kwa kawaida, Wayahudi wangeepuka kusafiri kupitia eneo la Samaria. Wasamaria walionekana kama watu wasiomcha Mungu kwa sababu walikuwa kizazi cha ufalme wa kaskazini mwa Israeli ambao walioana na wapagani. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/ungodly]], [[rc:///tw/dict/bible/other/kingdomofisrael]] and rc://*/ta/man/translate/figs-explicit)

Mahali sahihi pa ibada

Mojawapo ya dhambi kubwa zaidi zilizofanywa na watu wa Samaria katika historia ni kwamba walianzisha hekalu la uongo katika wilaya yao ili kushindana na hekalu huko Yerusalemu. Huu ndio mlima mwanamke anayezungumzia katika Yohana 4:20. Wayahudi walisema kwa haki kwamba Waisraeli wote waabudu huko Yerusalemu kwa sababu ndipo ambapo Yehova aliishi. Yesu anaelezea kwamba mahali pa hekalu hapajalishi tena. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/sin)

Mavuno

Taswira ya kuvuna hutumiwa katika sura hii. Hii ni mfano ambayo inawakilisha watu kuwa na imani katika Yesu. (See: [[rc:///ta/man/translate/figs-metaphor]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/faith]])

"Mwanamke Msamaria"

Mwanamke Msamaria labda ilitumika ili kuonyesha utofauti na hisia za Kiyahudi kumhusu Yesu. "Yesu mwenyewe alinena kwamba nabii hana heshima katika nchi yake" (Yohana 4:44). Kulikuwa na sababu nyingi ambazo Wayahudi wangeweza kumwona mwanamke huyu kama asiyeaminika. Alikuwa Msamaria, mzinzi, na mwanamke. Licha ya hii, alifanya kile alichohitaji Mungu. Alimwamini Yesu. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/prophet]], [[rc:///tw/dict/bible/kt/adultery]] and rc://*/tw/dict/bible/kt/believe)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Katika roho na kweli"

Ibada ya kweli haielekezwi tena kwa mahali moja, lakini sasa imeelekezwa kwake Yesu. Mbali na hayo, ibada haifanywi tena kwa kupitia makuhani. Kila mtu anaweza kumwabudu Mungu mwenyewe kwa njia ya moja kwa moja. Kifungu hiki kinamaanisha kwamba ibada sahihi kwa Mungu inaweza sasa kufanywa bila kutoa sadaka ya kuchinjwa na inaweza kufanywa kikamilifu kwa sababu ya ufunuo mkubwa uliotolewa kwa mwanadamu. Kuna ufahamu zaidi wa ziada wa kifungu hiki. Inaweza kuwa bora kuyaacha maneno haya kwa hali ya kawaida kama iwezekanavyo katika tafsiri ili kutoondoa maana nyingine iliyopo. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/reveal)

<< | >>