sw_tn/jdg/08/27.md

1.1 KiB

Gideoni akafanya efodi kutoka katika pete

"Gideoni alitumia dhahabu toka kwenye pete na kutengeneza efodi"

Ofra

Hili ni jina la mji.

Israeli wote wakaiandama kwa ukahaba na kuabudu

Kuabudu miungu ya uongo inafananishwa na ukahaba. "Waisraeli walimtenda Bwana dhambi kwa kuabudu efodi"

Waisraeli wote

Hii ni namna ya kusisitiza kuonesha kuwa idadi kubwa ya Waisraei waliabudu miugu.

Ilikuwa mtego kwa Gideoni na kwa wale walio nyumbani kwake.

Kuiabudu efodi inaelezwa kuwa ilikuwa mtego kwao. "ilikuwa jaribu kwa Gideoni na familia yake" au "Gideoni na familia yake walitenda dhambi kwa kuiabudu"

kwa wale walio nyumbani kwake

"nyumbani kwake" inawakilisha familia ya Gideoni.

Kwa hiyo Midiani ilishindwa mbele ya watu wa Israeli

Hii inaweza kuanza kama "Kwa hiyo Bwana akawafanya Wamidiani kushindwa mbele ya watu wa Israeli" au "kwa hiyo Bwana akawasaidia Waisraeli kuwashinda Wamidiani"

hawakuinua vichwa vyao tena

"Hawakuwavamia Waisraeli tena"

Na nchi ikawa na amani

"nchi" inawakilisha wana wa Israeli. "Na Waisraeli walikaa kwa amani"

Miaka arobaini

"miaka 40"

Siku za Gideoni

"siku" inamanisha kipindi cha uhai wake.