sw_tn/jdg/02/01.md

949 B

Malaika wa Bwana

yaweza kuwa na maana ya 1) "malaika anayemuwakilisha Bwana" au 2) "malaika anayemtumikia Bwana" au 3) yaweza kumaanisha Bwana mwenyewe, aliyeonekana kama malaika akiwa anazungumza na mtu.

akatoka Gilgali, akaenda Bokimu

"akaondoka Gilgali akaenda Bokimu"

Bokimu

Wana wa Irsaeli walipaita mahali hapa katika sura ya 2:5 baada ya malaika kuwakemea watu. "Bokimu" ina maana ya "kilio"

akasema

inaeleweka kuwa malaika wa Bwana alikuwa akizungumza na wana wa Israeli. "akasema na wana wa Israeli"

Nimekuleta kutoka Misri

"nimekutoa Misri"

Baba zako

"mababu zako"

kuvunja agano langu na wewe

"kushindwa kufanya yale niliyopaswa kufanya kwako"

Haukuisikiliza sauti yangu

"sauti" ina maanisha alichokisema Bwana. "haukusikiliza ammri zangu"

Ni nini hiki ulichokifanya?

Swali hili linaulizwa ili kuwafanya wana wa Israeli wagundue kuwa hawajamtii Mungu na watateseka kwa sababu hiyo. "Mmefanya jambo baya"