# Malaika wa Bwana yaweza kuwa na maana ya 1) "malaika anayemuwakilisha Bwana" au 2) "malaika anayemtumikia Bwana" au 3) yaweza kumaanisha Bwana mwenyewe, aliyeonekana kama malaika akiwa anazungumza na mtu. # akatoka Gilgali, akaenda Bokimu "akaondoka Gilgali akaenda Bokimu" # Bokimu Wana wa Irsaeli walipaita mahali hapa katika sura ya 2:5 baada ya malaika kuwakemea watu. "Bokimu" ina maana ya "kilio" # akasema inaeleweka kuwa malaika wa Bwana alikuwa akizungumza na wana wa Israeli. "akasema na wana wa Israeli" # Nimekuleta kutoka Misri "nimekutoa Misri" # Baba zako "mababu zako" # kuvunja agano langu na wewe "kushindwa kufanya yale niliyopaswa kufanya kwako" # Haukuisikiliza sauti yangu "sauti" ina maanisha alichokisema Bwana. "haukusikiliza ammri zangu" # Ni nini hiki ulichokifanya? Swali hili linaulizwa ili kuwafanya wana wa Israeli wagundue kuwa hawajamtii Mungu na watateseka kwa sababu hiyo. "Mmefanya jambo baya"