sw_tn/jas/05/07.md

28 lines
772 B
Markdown

# Sentensi unganishi
Yakobo anabadilisha mada toka kwenye kuwakemea matajiri na kuwapa mawaidha waamini.
# Maelezo ya jumla
Kwa kufunga Yakobo anawakumbusha waamini kuhusu ujio wa Bwana na kuwapa mafundisho mafupi namna ya kuishi kwa ajili ya Mungu.
# Kwa hiyo vumilieni
"Kwa ajili ya hili kuweni na subira na uvumilivu"
# mpaka ujio wa Bwana
Sentensi hii inaelezea ujio wa Yesu, atakapoanzisha ufalme wake duniani na kuhukumu watu wote. "Mpaka Kristo atakapokuja"
# Mkulima
Katika mazungumzo haya Yakobo anatumia mkulima na mwamini kuelezea namna ya kuwa mvumilivu.
# Kazeni mioyo yenu
Yakobo anawataka waamini wawe na mioyo thabiti na kuwa na msimamo. "Kuweni na msimamo" au "Ifanyeni imara mioyo yenu"
# kuja kwake Bwana ni karibu.
"Bwana atarudi mapema"