sw_tn/isa/63/17.md

16 lines
764 B
Markdown

# Maelezo ya Jumla
Watu wa Israeli wanaendelea kuzungumza.
# Yahwe, kwa nini unatufanya tuzurure kutoka katika njia zako na kuifanya mioyo yetu kuwa migumu, ili kwamba tusikutii wewe?
Hapa mwandishi anatumia swali kuelezea lalamiko la watu wa Mungu. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Yahwe umetufanya tuzurure kutoka katika njia zako na kuwa wakaidi ili kwamba tusikutii"
# kwa nini unatufanya tuzurure kutoka katika njia zako
Kutofanya kile ambacho Yahwe anaamuru inazungumziwa kana kwamba mtu anazurura kutoka katika njia sahihi. "kwa nini unatufanya kufanya kilicho kibaya"
# kuifanya mioyo yetu kuwa migumu
Hii ina maana kutoweza kukataa mafundisho ya Yahwe kwa kukataa kusikiliza na kutii. Hapa "moyo" unawakilisha nia, hisia na shauku zao.