sw_tn/isa/60/04.md

24 lines
756 B
Markdown

# Maelezo ya Jumla
Hapa Yahwe anaanza kuzungumza.
# Wote wanajikusanya
"Wote" ina maana ya watu waliobakii wa Israeli ambao watakuja pamoja kurudi Yerusalemu.
# binti zako watabebwa mikononi mwao
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watabeba binti zako mikononi mwao" au "watabeba binti zako juu ya viuno vyao"
# Kisha utatazama na kung'aa, na moyo wako utashangilia na kumwagikia
Misemo hii inatumia maana moja na kusisitiza ya kwamba watakuwa na furaha sana kwa sababu ya kile kitakachotokea Yerusalemu.
# wingi wa bahari
Hii ina maana ya utajiri na bidhaa ambazo zitakuja Yerusalemu kwa njia ya meli, labda kupitia Bahari ya Mediteranea.
# utamwagwa nje kwako
Hii inaelezea ya kwamba wingi utakuwa kama maji ambayo yanabubujika nje.