# Maelezo ya Jumla Hapa Yahwe anaanza kuzungumza. # Wote wanajikusanya "Wote" ina maana ya watu waliobakii wa Israeli ambao watakuja pamoja kurudi Yerusalemu. # binti zako watabebwa mikononi mwao Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watabeba binti zako mikononi mwao" au "watabeba binti zako juu ya viuno vyao" # Kisha utatazama na kung'aa, na moyo wako utashangilia na kumwagikia Misemo hii inatumia maana moja na kusisitiza ya kwamba watakuwa na furaha sana kwa sababu ya kile kitakachotokea Yerusalemu. # wingi wa bahari Hii ina maana ya utajiri na bidhaa ambazo zitakuja Yerusalemu kwa njia ya meli, labda kupitia Bahari ya Mediteranea. # utamwagwa nje kwako Hii inaelezea ya kwamba wingi utakuwa kama maji ambayo yanabubujika nje.