sw_tn/isa/52/02.md

20 lines
877 B
Markdown

# Maelezo ya Jumla
Isaya anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli.
# Jikung'ute kutoka mavumbini; amka na ukae, Yerusalemu
Hapa "Yerusalemu" inawakilisha watu wanaoishi kule. "Watu wa Yerusalemu, simama wima na ukung'ute uchafu kutoka kwako"
# ondoa mnyororo kutoka shingoni mwako, mfungwa
Inaonyeshwa ya kwamba watu wa Yerusalemu walikuwa wakivaa minyororo kwa sababu walikuwa watumwa walipokuwa uhamishoni Babeli. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi.
# binti Sayuni
Hii ni lahaja. "binti" wa mji ina maana watu wa mji ule. "watu wa Sayuni" au "watu ambao wanaishi Sayuni"
# Uliuzwa bure, na utakombolewa bila fedha
Hii inazungumzia kuhusu Yahwe kana kwamba alikuwa mmiliki wa watu wa Israeli. Kwa kuwa ni mmiliki halali anaweza kuwatoa au kuwarudisha atakavyotaka. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. :Nimekuuza bure, na nitakukomboa bila fedha"