sw_tn/isa/48/09.md

20 lines
798 B
Markdown

# Maelezo ya Jumla
Yahwe anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli
# Kwa ajili ya jina langu nitasitisha hasira yangu
Hapa neno "jina" lina maana ya sifa ya Yahwe. "Kwa ajili ya sifa yangu nitakawiza hasira yangu"
# na kwa ajili ya heshima yangu nitajizuia kukuangamiza
Sehemu hii ya sentensi ina maana moja kama sehemu ya kwanza.
# Tazama, nilikutakasa, lakinii sio kama fedha; nimekutakasa katika tanuu la mateso
Yahwe anazungumzia kutumia mateso kusafisha watu wake kana kwamba walikuwa vyuma vya thamani na mateso yalikuwa tanuu ambano anawatakasa.
# kwa kuwa ninawezaje kuruhusu jina langu kudharauliwa?
Yahwe anatumia swali kusisitiza kuwa hawezi kuruhusu jina lake mwenyewe kudharauliwa. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "kwa maana sitaruhusu yeyote kudharau jina langu"