sw_tn/isa/47/01.md

28 lines
963 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla
Katika sura hii, Yahwe anazungumza na Babeli kuhusu anguko lake kana kwamba alikuwa malkia ambaye ameaibishwa.
# keti katika vumbi, binti bikira wa Babeli; keti juu ya ardhi ... binti wa Wakaldayo.
Misemo hii miwili ina maana moja. Kuketi katika mavumbi ni ishara ya aibu.
# binti bikirawa Babeli ... binti wa Wakaldayo
Misemo hii miwili ina maana ya mji, Babeli, ambao unazungumziwa kana kwamba ilikuwa binti. Ya kwamba mji ni "binti" ikionyesha jinsi watu wanavyofikiri kwa kubembeleza juuyake.
# bila kiti cha enzi
Hapa "kiti cha enzi" ina maana ya nguvu ya kutawala. "bila nguvu ya kutawala"
# Hautaitwa tena mrembo na wa kuvutia
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Watu hawatakuita tena mrembo na wa kuvutia"
# mrembo na mzuri
Maneno haya mawili yanatumia maana moja. Wanafafanua yule ambaye ni mzuri na anaishi katika starehe. "mzuri sana" au "mwenye starehe sana"
# jiwe la kusaga
jiwe kubwa linatumiwa kusaga nafaka