sw_tn/isa/40/09.md

24 lines
883 B
Markdown

# Panda katika mlima wa juu, Sayuni, mletaji wa habari njema
Mwandishi anazungumzia Sayuni kana kwamba ilikuwa mjumbe anayetmka habari njema kutoka katika kilele cha mlima.
# Panda katika mlima wa juu
Wajumbe mara kwa mara husimama juu ya nchi iliyoinuka, kama vile milima, ili kwamba watu wengi waweze kusikia kile walichotangaza.
# Sayuni
Hii ina maana ya watu ambao wanaishi Sayuni. "nyie watu wa Sayuni"
# Yerusalemu. Wewe uletaye habari njema
Mwandishi anazungumzia Yerusalemu kana kwamba ilikuwa mjumbe ambaye hutangaza habari njema.
# na mkono wake wa nguvu hutawala kwa ajili yake
Hapa neno "mkono" linawakilisha nguvu ya Mungu. "na anatawala kwa nguvu kubwa"
# dhawabu yake ipo pamoja naye ... wale ambao amewaokoa huenda mbele zake
Misemo hii miwili ina maana moja. Wale ambao aliwaokoa ni "zawadi" yake. "anawaleta wale aliowaokoa pamoja naye kama zawadi yake"