sw_tn/isa/35/01.md

28 lines
1.5 KiB
Markdown

# Nyika na mahali penye ukiwa patafurahi; na jangwa litashangilia
Misemo hii miwili kimsingi iuna maana moja. Sehemu hizi inaelezwa kama kuwa na furaha, kama mtu anavyokuwa na furaha, kwa sababu zimepokea maji na zinachanua. "Itakuwa kama nyika na mahali penye ukiwa pana furaha na jangwa litashangilia"
# na kuchanua
Hii inazungumzia mimea katika jangwa kuchanua kana kwamba jangwa lenyewe lilikuwa likichanua. "na mimea yake itachanua"
# Kama waridi, litachanua kwa wingi
Hii inalinganisha namna ya mimea ya jangwa huchanua kwa namna ambavyo waridi unavyochanua kwa wingi. "Jangwa litaota mimea na miti mipya mingi"
# na kushangilia kwa furaha na kuimba
Hii inazungumzia jangwa kana kwamba ilikuwa na furaha na kuimba kama mtu. "itakuwa kana kwamba kila kitu kinashangilia na kuimba!"
# utukufu wa Lebanoni utapewa kwake
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. Hii inazungumzia Yahwe kulifanya jangwa kuonekana na utukufu kama wa Lebanoni kana kwamba alikuwa akilipa jangwa utukufu wa Lebanoni. "Yahwe ataupatia Lebanoniu utukufu wake" au "Yahwe ataufanya uwe mzuri kama Lebanoni"
# uzuri wa Karmeli na Sharoni
Maneno ambayo hayapo yanaweza kuongezwa. Pia, hii inamzungumzia Yahwe kulifanya jangwa kuonekana zuri kama Karmeli na Sharoni kana kwamba alikuwa akilipa jangwa uzuri wake. "uzuri wa Karmeli na Sharoni utapewa kwake" au "Yahwe ataufanya uwe mzuri kama Karmeli na Sharoni"
# utukufu wa Yahwe, uzuri wa Mungu wetu
Misemo hii miwili kimsingi ina maana moja na inasisitiza kutokea kwa Yahwe.