sw_tn/isa/34/11.md

32 lines
969 B
Markdown

# wataishi kule
"wataishi katika nchi ya Edomu"
# bundi
Bundi ni ndege pori wanaowinda usiku
# kunguru
Huyu ni ndege mkubwa mweusi. Ni vigumu kutambua baadhi ya aina haswa za ndege zinazotajwa katika sehemu hii. Hata hivyo, wote walikuwa ndege ambao walipendelea kuishi katika maeneo ambayo hapakuwa na watu, kwa hiyo waliashiria sehemu zilizotelekezwa.
# ndani mwake
"kule". Hii ina maana ya Edomu.
# Naye atanyosha juu yake kamba ya kupimia ya uharibifu na timazi ya uvunjifu
Hii inamzungumzia Yahwe kana kwamba alikuwa mjenzi mwangalifu kama akisababisha uharibifu katika Edomu. "Yahwe atapima nchi kwa uangalifu; atapima kuamua wapi kusababisha uharibifu na uvunjifu"
# kamba ya kupimia ... timazi
Hivi ni vifaa vya mjenzi.
# Waadilifu wake ... wakuu wake
"Waadilifu wa Edomu ... wakuu wa Edomu"
# wakuu wake wote hawatukuwa kitu
Hii inakuza kuhusu wakuu kupoteza nafasi yao ya ufalme kwa kusema watakuwa si kitu. "wakuu wake wote hawatatawala tena"