sw_tn/isa/30/12.md

36 lines
1.2 KiB
Markdown

# Mtakatifu wa Israeli
Mtakatifu wa Israeli
# unakataa neno hili
Hapa "neno" inawakilisha ujumbe. "unakataa ujumbe huu"
# kuamini katika ukandamizaji na udanganyifu na kuiegemea
Maana zaweza kuwa 1) viongozi wa Yuda wanaamini katika viongozi wa Misri mbao hutawala kwa kukandamiza na kudanganya wengine au 2) viongozi wa Yuda wamekandamiza na kudanganya watu wao wenyewe ili kuchukua fedha zao na kuituma kwa viongozi wa Misri kama malipo kwa ajili ya ulinzi.
# kuiegemea
Hapa neno "kuiegemea" ina maana ya "ukandamizaji na udanganyifu". "kuziegemea"
# egemea katika
Hii ni lahaja ambayo ina maana ya kuamini au kutegemea juu ya kitu.
# kwa hiyo dhambi hii kwako itakuwa kama sehemu iliyovunjika ... kwa mara moja
Tashbihi hii ina maana ya kwamba Mungu ataangamiza watu wa Yuda ghafla kwa sababu ya dhambi zao.
# kama sehemu iliyovunjka tayari kudondoka
Inaeleweka ya kwamba hii ni sehemu iliyovunjika ya ukuta. "kama sehemu iliyovunjika ya ukuta ambayo iko tayari kuanguka"
# ambao anguko lake litatokea ghafla
Hii inaweza kundikwa ili kwamba nomino dhahania "anguka" inaelezwa kama kitenzi "anguka". "ambayo itaanguka ghafla"
# ghafla, kwa mara moja
Hizi zina maana ya kitu kimoja na husisitiza jinsi ukuta utakavyoanguka kwa haraka.