sw_tn/isa/22/05.md

36 lines
1.2 KiB
Markdown

# Kwa maana kuna siku
Hapa "siku" ina maana ya kipindii kirefu cha muda. "Kwa maana kutakuwa na muda"
# ya ghasia, kukanyagwa chini, na kuchanganyikiwa kwa ajili ya Bwana, Yahwe wa majeshi
"pale Yahwe wa majeshi atasababisha hofu kubwa, kukanyagwa chini, na kuchanganyikiwa
# kukanyagwa chini
Maana zaweza kuwa 1) hii ina maana ya wanajeshi wakitembea au 2) watu kwa ujumla wanakimbia kwa hofu kubwa na kutokuwa na uhakika wapi pa kwenda.
# katika Bonde la Maono
Hapa "Bonde" ina maana ya wale ambao wanaishi katika bonde, yaani, Yerusalemu. "juu ya wale ambao wanaishi katika Bonde la Maono" au "kuhusu wale ambao wanaishi Yerusalemu"
# watu kulia katika milima
Maana zaweza kuwa 1) "watu katika milima watasikia sauti zao" au 2) "milio ya watu inasikika katika milima"
# Elamu anabeba podo
Podo ni mfuko wa kubeba mishale na inawakilisha silaha za mpiga mshale. "Wanajeshi wa Elamu huchukua upinde zao na mishale"
# Kiri anaweka wazi ngao
Hapa "Kiri" inawakilisha wanajeshi. "wanajeshi wa Kiri watabeba ngao zao nje ya makasha yao"
# Kiri
Kiri ni mji wa Media.
# mabonde yako mazuri
Hapa "yako" ina maana ya watu wa Yerusalemu. Isaya hajijumlishi mwenyewe kama mmoja wa watu wa Yerusalemu. "mabonde yetu mazuri"