sw_tn/isa/17/01.md

36 lines
1.3 KiB
Markdown

# kuhusu Dameski
Dameski ni jina la mji.
# miji ya Aroeri itatelekezwa
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Watu wote watatelekeza miji ya Aroeri"
# hakuna atakayewatisha
Neno "atakayewatisha" ina maana ya kondoo
# Miji iliyoimarishwa itatoweka kutoka Efraimu
Efraimu ilikuwa kabila kubwa zaidi la Israeli. hapa linawakilisha ufalme wote wa kaskazini wa Israeli. "Miji imara itatoweka kutoka Israeli"
# itatoweka
Hii haimaanishi ya kwamba zitapotelea, lakini miji ile itaangamizwa.
# ufalme wa Dameski
Maneno "itatoweka" inaeleweka kutoka kwa msemo uliopita. Dameski ilikuwa mahali ambapo mfalme wa Aramu alitawala. Ufalme kutoweka unawakilisha mflame kutokuwa tena na nguvu za kifalme. "ufalme utatoweka kutoka Dameski" au "hapatakuwa na nguvu ya kifalme Dameski"
# Aramu
Aramu ni jina la taifa.
# watakuwa kama utukufu wa watu wa Israeli
Kwa kuwa watu wa Israeli hawakuwa na utukufu tena, hii ilimaanihsa ya kwamba waliosalia wa Aramu hawatakuwa na utukufu tena. "hawatakuwa na utukufu tena, kama watu wa Israeli" au "Nitaleta aibu juu yao kama nilivyofanya kwa watu wa Israeli"
# tamko la Yahwe wa majeshi
Hii inaweza kuandikwa upya ili kwamba nomino dhahania "tamko" ielezwe kama kitenzi "alitamka" au "alisema kwa dhati". "Hivi ndivyo Yahwe wa majeshi alivyotamka" au "hivi ndivyo Yahwe wa majeshi alivyosema kwa dhati".