sw_tn/gen/41/12.md

40 lines
1.0 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Mkuu wa wanyweshaji anaendelea kuzungumza na Farao.
# Pamoja nasi kulikuwa
"Gerezani kulikuwa na mkuu wa waokaji na mimi"
# kapteni wa walinzi
Askari msimamizi wa walinzi wa kifalme.
# Tulimwambia na akatutafsiria ndoto zetu
"Tulimwambia ndoto zetu na kutueleza maana zake kwetu"
# Alitutafsiria kila mmoja wetu kulingana na ndoto yake
Hapa "yake" ina maana ya mnyweshaji na muokaji mmoja mmoja, sio kwa yule anayetafsiri ile ndoto. "Alifafanua kile kilichokuwa kinakuja kutokea kwetu wawili"
# Ikawa
Msemo huu unatumika kuweka alama ya tukio muhimu la simulizi.
# alivyotutafsiria, ndivyo ilivyokuwa
"alivyotafsiri kuhusu ndoto ndivyo kilichotokea hapo baadae"
# Farao alinirudisha katika nafasi yangu
Hapa mnyweshaji anatumia jina la Farao katika kuongea naye kama njia ya kumheshimu yeye. "Uliniruhusu nirudi katika kazi yangu!"
# yule mwingine
"mkuu wa waokaji"
# akamtundika
Hapa "akamtundika" ina maana ya Farao. Na ina maana ya maaskari ambao Farao aliwaamuru kumnyonga mkuu wa waokaji. "uliwaamuru maaskari wako kumnyonga"