sw_tn/gen/29/07.md

32 lines
823 B
Markdown

# ni mchana
"jua bado lipo juu angani" au "jua bado linawaka kwa mwanga"
# wakati wa kukusanya kondoo pamoja
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kwako kukusanya mifugo"
# kukusanya pamoja
Hii ina maana ya kuwakusanya pamoja ndani ya uzio ili wakae kwa usiku. Maana kamili ya hii inaweza kuwekwa wazi.
# kuwaacha wachunge
"waache wale nyasi shambani"
# Hatuwezi kuwanywesha
"Inatubidi kusubiri ili kuwanywesha". Hii inahusu suala la muda, na sio ruhusa.
# Hatuwezi kuwanywesha mpaka makundi yote yakusanyike pamoja
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "hadi pale wafugaji wengine watakapokusanya mifugo yao"
# kutoka mlangoni mwa kisima
Hapa "mlangoni" ni njia ya kuelezea uwazi. "kutoka kwa kisima" au "kutoka kwa uwazi wa kisima"
# na ndipo tutakapowanywesha kondoo
"kisha tutawanywesha kondoo"