# ni mchana "jua bado lipo juu angani" au "jua bado linawaka kwa mwanga" # wakati wa kukusanya kondoo pamoja Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "kwako kukusanya mifugo" # kukusanya pamoja Hii ina maana ya kuwakusanya pamoja ndani ya uzio ili wakae kwa usiku. Maana kamili ya hii inaweza kuwekwa wazi. # kuwaacha wachunge "waache wale nyasi shambani" # Hatuwezi kuwanywesha "Inatubidi kusubiri ili kuwanywesha". Hii inahusu suala la muda, na sio ruhusa. # Hatuwezi kuwanywesha mpaka makundi yote yakusanyike pamoja Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "hadi pale wafugaji wengine watakapokusanya mifugo yao" # kutoka mlangoni mwa kisima Hapa "mlangoni" ni njia ya kuelezea uwazi. "kutoka kwa kisima" au "kutoka kwa uwazi wa kisima" # na ndipo tutakapowanywesha kondoo "kisha tutawanywesha kondoo"