forked from WA-Catalog/sw_tn
33 lines
1.1 KiB
Markdown
33 lines
1.1 KiB
Markdown
# Abimeleki akamwita Isaka kwake
|
|
|
|
Yawezekana Abimeleki alimtuma mtu kumwambia Isaka ya kwamba alihitaji kumuona. "Abimeleki alimtuma mtu kumleta Isaka kwake"
|
|
|
|
# Kwa nini ulisema, 'Yeye ni dada yangu?"
|
|
|
|
Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuelezwa kama nukuu isiyokuwa moja kwa moja. "Kwa nini ulisema ya kwamba ni dada yako?"
|
|
|
|
# amchukue
|
|
|
|
"ili amchukue"
|
|
|
|
# Ni jambo gani hili ulilotufanyia?
|
|
|
|
Abimeleki alitumia swali hili kumkaripia Isaka. "Haukupaswa kufanya jambo hili kwetu!"
|
|
|
|
# ungeweza kuleta hatia juu yetu
|
|
|
|
Hii inazungumzia kuhusu kumsababisha mtu kuwa na hatia kana kwamba "hatia" ilikuwa ni kitu kinachowekwa juu ya mtu. "ungeweza kusababisha tuwe na hatia ya kuchukua mke wa mtu"
|
|
|
|
# juu yetu
|
|
|
|
Hapa "yetu" ina maana ya Abimeleki na watu wake.
|
|
|
|
# Mtu yeyote atakayemgusa mtu huyu
|
|
|
|
Hapa "atakayemgusa" ina maana ya kumgusa kwa namna ya kumdhuru. "Yeyote atakayemdhuru mwanamume huyu"
|
|
|
|
# hakika atauwawa
|
|
|
|
Inawezekana Abimeleki alikusudia kumwambia mtu kumuua yeyote ambaye angemdhuru Isaka au Rebeka.
|
|
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Nitamuua" au "Nitawaamuru wanamume wangu kumuua"
|