sw_tn/gen/24/31.md

32 lines
1000 B
Markdown

# Njoo
"Njoo ndani" au "Ingia"
# uliye barikiwa na Yahwe
"wewe ambaye Yahwe amekubariki"
# uliye
Hapa neno la "uliye" lina maana ya mtumishi wa Abrahamu.
# Kwa nini umesimama nje?
Labani alitumia swali hili kumkaribisha mtumishi wa Abrahamu katika nyumba yake. Swali hili linaweza kutafsiriwa kama kauli. "Hauhitaji kubaki nje"
# Kwa hiyo yule mtu akaingia ndani ya nyumba
Neno "akaingia" linaweza kutafsiriwa kama "akaenda"
# kashusha mizigo kutoka kwa wale ngamia
Haipo wazi nani alifanya kazi hii. Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mtumishi wa Labani alishusha mizigo kutoka kwa ngamia" au "ngamia walishushwa mizigo"
# Ngamia wakapatiwa malisho na chakula, na maji yakatolewa
Hii haisemi nani alifanya kazi hii. Iwapo utaweka hii katika hali ya kutenda basi sema "watumishi wa Labani" kama jambo. "Watumishi wa Labani waliwapa malisho na chakula ngamia, na wakatoa maji"
# kuosha miguu yake ... naye
"kwa watumishi wa Abrahamu na wanamume waliokuwa naye kuosha miguu yao"