sw_tn/gen/21/22.md

48 lines
1.3 KiB
Markdown

# Ikawa kwamba katika wakati ule
Msemo huu unaweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.
# Fikoli
Hili ni jina la mwanamume.
# kamanda wa jeshi lake
"kamanda wa jeshi lake"
# jeshi lake
neno "lake" lina maana ya Abimeleki.
# Mungu yuko pamoja na wewe katika yote uyatendayo
Hapa msemo "yuko pamoja nawe" ni lahaja yenye maana ya Mungu husaidia au humbariki Abrahamu. "Mungu hubariki kila kitu ufanyacho"
# Sasa basi
Neno "Sasa" halimaanishi "katika muda huu", lakini linatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata. "Sasa basi"
# niapie hapa kwa Mungu
Hii ni lahaja yenye maana ya kutoa kiapo cha dhati kinachoshuhudiwa na mamlaka ya juu, kwa hali hii ni Mungu. "niahidi mimi na Mungu kama shahidi"
# kwamba hutanifanyia baya
"ya kwamba hutanidanganya"
# kwamba hutanifanyia baya ... pamoja na uzao wangu
Hii inaweza kuelezwa kwa njia ya chanya. "utanifanyia haki mimi na uzao wangu"
# Onesha kwangu ... gano lile lile la uaminifu ambalo nimekuonesha wewe
Wanamume wawili walifanya agano kati yao. Kitenzi kinachojitegemea "umaninifu" kinaweza kuelezwa kama "mwaminifu" au "mtiifu". "Uwe mwaminifu kwangu na kwa nchi kama nilivyokuwa kwako"
# kwa nchi
Hapa "nchi" ina maana ya watu. "kwa watu wa nchi"
# nina apa
Hii inaweza kuelezwa kwa taarifa iliyoeleweka. "Ninaapa kuwa mwaminifu kwako na kwa watu wako kama ulivyokuwa kwangu"