sw_tn/gen/08/06.md

20 lines
696 B
Markdown

# Ikatokea kwamba
Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi. "Ikawa kwamba"
# Ikatokea kwamba ... dirisha la safina ambayo aliitengeneza
Msemo "ambayo alitengeneza" unazungumzia kuhusu madirisha. Baadhi ya lugha zaweza kufanya msemo huu kuwa sentensi tofauti. "Nuhu alitengeneza dirisha katika safina. Ikaja kuwa baada ya siku arobaini ndipo dirisha likafunguliwa"
# kunguru
ndege mweusi anayekula zaidi nyama ya mizoga ya wanyama
# akaruka mbele na nyuma
Hii ina maana ya kwamba kunguru aliendelea kuacha safina na kurejea.
# hadi maji yalipo kauka
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "hadi pale upepo ulipokausha maji" au "hadi maji yalipokauka"