sw_tn/gen/07/13.md

20 lines
731 B
Markdown

# Taarifa ya jumla
Mistari ya 13-18 inarudia kwa mara ya tatu na kutoa kwa undani kuhusu jinsi gani Nuhu aliingia katika safina pamoja na familia yake na wanyama katika 7:1. Hili si tukio jipya.
# Katika siku iyo hiyo
"Katika siku hiyo hasa". Hii ina maana ya siku ambayo mvua ilianza kunyesha. Mistari ya 13-16 inaeleza Nuhu alichofanya kabla tu ya mvua kuanza.
# mnyama wa mwitu ... mnyama wa kufugwa ... kila kitambaacho ... ndege
Vikundi hivi vinne vinaorodheshwa kuonyesha ya kwamba kila aina ya mnyama alijumuishwa.
# kila kitambaacho
Hii ina maana ya wanyama watambaao juu ya ardhi, kama wanyama wagugunaji, wadudu, mjusi na nyoka.
# kwa jinsi yake
"ili kwamba kila aina ya mnyama azalishe zaidi ya kila aina yake"